26 Novemba 2024 - 19:34
"Haaretz" iliripoti; Maelfu ya Wazayuni walikimbilia Canada katika kivuli cha vita

Gazeti la Kizayuni la "Haaretz" lilitangaza kuwa, idadi ya Waisraeli wanaohamia Canada imeongezeka sana.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Gazeti la Kizayuni la "Haaretz" limetangaza ongezeko kubwa la idadi ya Wazayuni wanaohamia Canada kutoka katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina.

Gazeti hili la Kizayuni limesema kuwa sababu ya kuhama Wazayuni hao ni kuendelea vita na uvunjifu wa demokrasia.